Bwana Mungu, nashangaa kabisa Nikitazama kama vilivyo Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote viumbwavyo kwa uwezo wako. Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu. Nikitembea pote duniani, Ndege huimba, nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia. Nikikumbuka kama Wewe Mungu Ulivyompeleka Mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno. Yesu Mwokozi utakaporudi Kunichukua kwenda Mbinguni, Nitashukuru na kuimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo.Como las olas del profundo mar سبحوه مجدوه Il segreto della mia allegria ليك كل الحمد Kutsal, Kutsal nǐ zhè shòu kùn kǔ Vládni mi Men bilan boʻlgin أريد ان ابرء Zanech nářku, přestaň zoufat
Song not available - connect to internet to try again?