Bwana uliyewaita Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako; wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa. Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza tena Ni nani aliyeko Atakaye nimtume Afundishe vijana? 'Ni tayari, Bwana wangu, Nitume mimi Bwana.' Nitume na mimi, Bwana Kama ulivyotumwa, Habari ya msamaha Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na waliopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia. Astahiliye hapana Kutamka habari, Lakini wewe waweza Kutufanya tayari. Neno lako tulijue, Tupe na roho yako, Hayatakuwa ya bure, Haya maneno yako.Trust По дорогам и вдоль изгородей sẖạyf ạ̹ydyk Ty mi dávaš nádej ạ̉nạ byk mnṣwr Все вперед Все вперед 我们带着天上的异象 Как солнце едино над нами Misy ny fonenana Отчизна моя дорогая
Song not available - connect to internet to try again?