Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia? Unateseka sana, Kwa ajili ya kuomba, Waomba na jasho jingi likageuka damu. Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, Mimi leo, naja kwako Ili niziungame. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia, na mizigo mizito? Umejitwalia wewe, msalaba mabegani Kwa ajili ya watu. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi, Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe, Chukua roho yangu. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Muda ulipofika, nchi ikawa giza, Mbinguni pakatulia, Angani pakawa kimya, Watu wakaogopa. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba, Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni, Naimba, Haleluya.Missão Esperança ميدلي 1 Хич ким Сең ялы дәл bnyjy wntwạḍʿ qdạmk Himak nitak á, ahanchi Tisíc ráz buď nami ctená, Mária od anjelov pozdravená Kráľovná Տեր Ինչ Գեղեցիկ ես 要把财宝积攒在天上 Вечер Лодка Середина моря Небесная родина
Song not available - connect to internet to try again?