Mapenzi yako yafanyike, Wewe mfinyanzi, nami towe, Unifinyange upendavyo, Mimi tayari, naja kwako. Mapenzi yako yafanyike, Unihoji dhambi zote, Unisafishe vya kimwili, Niinamapo Msalabani. Mapenzi yako yafanyike, Mimi dhaifu, mimi mnyonge. Uwezo wote, kwako kweli, Sasa niponye, Ee, Mwokozi. Mapenzi yako yafanyike, Natoa kwako vitu vyote, Maisha, mali, moyo, mwili, Vyote ni vyako, kweli, kweli. Mapenzi yako yafanyike, Mapenzi yangu yavunjike, Ninakubali uwe Bwana, Ni mali yako, twaa kabisa. Mapenzi yako yafanyike, Unitawale siku zote, Sura ya Yesu umba kwangu, Nijaze Roho nayo nguvu.Náš Pán lék vždy má Romalılar 11:33+36 O herr giesse strome Мəним үчүн гызылдан да баһа Ry fitiavan'i Jesosy NGAI LAW ZUM TUAH من حبك خليتني ابنك Stačí sa nadýchnuť Ogni parte di me Ko Zan Tafi da Hannu Wofi
Song not available - connect to internet to try again?