Msingi imara, enyi wa kweli, Umekwisha pigwa kwa neno hili; Aongeze lipi? Mnayo pia Kwa Yesu mliomkimbilia. Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka taipunguza; Takupa nawe, nikuwezeshe, Ipata kufaa, isikutishe! Utakapopishwa ndani ya moto Nnguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako, Na zitasalia dhahabu zako. Hata zije mvi, walio wangu Hawaoni kwisha mapenzi yangu; Nazo zitakapowenea, ndipo Mabegani mwangu niwatwekapo. Na mtu aliyenitegemea Kamwe kwa adui sitamtia; Nguvu za jehanam zijapotisha, Mtu wangu kamwe sitamuacha.Рахмат сиңа Аллам พระเจ้าเป็นความรัก 耶和华用大能的手 أتكل عليك Герои веры Jeg vil rope det ut Меня Ты возлюбил نظرت من السماء FOUNTAIN OF LIFE zhǔ wǒ lái dào nǐ miàn qián
Song not available - connect to internet to try again?