1. Mwamba uliopasuka, ndani yako nijifiche! Maji yale, damu ile itokayo mbavu zako, iwe dawa ya kuponya roho yangu na ubaya! 2. Kazi za mikono yangu, haziwezi kukomboa. Hata ningelia sana na kutenda kazi nyingi, singeweza kuokoka, peke yako u Mwokozi. 3. Ndani yangu sina kitu, naushika msalaba. Uchi mimi, univike! Sina nguvu, nichukue! Ni mchafu, unioshe! Wewe u Mwokozi wangu. 4. Kwa maisha yangu yote hata nitatoa roho, hata saa ya kuitwa mbele ya Mfalme wangu, mwamba uliopasuka, nijifiche ndani yako!Busca primero el reino de Dios Iata ce vorbeşte Domnul Celebrate il Signore БОГ ВСЕМОГЪЩ Oči svoje už zavieram, k spánku sa ukladám yạ mw̉mn ạ̉sẖhd wsṭ ạlʿạlm Ийи Чобан Баарынан эң жогору Звёзды умирают и рождаются Shekinah
Song not available - connect to internet to try again?