Ni siku kuu siku ile Ya kumkiri Mwokozi! Moyo umejaa tele, Kunyamaza hauwezi. Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu. Tumekwisha kupatana Mimi wake, yeye wangu, Na sasa nitamwandama, Nikiri neno la Mungu. Moyo tulia kwa Bwana Kiini cha raha yako, Huna njia mbili tena; Yesu ndiye njia yako. Nadhiri yangu ya mbele Nitaiweka daima, Hata ije siku ile, Ya kuonana kwa salamaApostoli hitvallás I looked over Jordan إلقاء 4 Czemu rozpaczasz we mnie Merci pour ton amour Świeć Jezu świeć Я иду из далека Il canto nella prigione چووچۇنداردى چوعۇلتۇپ Я хочу служить только лишь Тебе
Song not available - connect to internet to try again?