Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nilikupa miaka Yangu duniani Upate inuka, Kuishi Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini: Niliacha nuru Za Baba, Mbinguni, Kwingia taabu Za ulimwenguni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Niliteswa sana, Mateso kifoni, Usije yaona Hayo ya motoni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nimekuletea Huku duniani Upendo na afya Zatoka Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nipe siku zako, Udumu mwangani; Na taabu yako, Wingie rahani Nafsi, pendo, mali, Twae Imanweli.Grace Like Rain في عالم الدموع Каждый благословен Серебряный дождь Do górnej ojczyzny pociąga mię stąd Радость от Тебя Дюнямъз Шашкъндъ اتكلم گِل، واقت بُلدی، آلقیشلامانا Всему свое время
Song not available - connect to internet to try again?