Nilikuwa kondoo aliyepotea, Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea Nilikuwa mwana asiyesikia, Sikupenda baba yangu wala kutulia. Na mchunga mwema alinitafuta, Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta; Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa, Waliniona mnyonge, waliniokoa. Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana, Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana; Kwa vidonda vyangu alitia dawa. Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa. Nilikuwa kondoo aliyepotea Sasa nampenda Baba, na mchunga pia; Kwanza nilitanga na kukosa sana, Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.Если любишь Иисуса Я нуждаюсь в Иисусе Он меня простил Když se světem loudáš sám - manželská verze Oh, Señor, maravilloso eres Tú Entrons dans sa présence 神悦纳的禧年 Манъа келинъ эр кес Je m'approche de toi qlby ạ̉syr nʿmtk Maelfu Na Maelfu
Song not available - connect to internet to try again?