Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Moyo ulionyunyizwa Damu ya thamani. Moyo msikizi, moyo Wa kunyenyekea, Moyo utawaliwao Na Mwokozi pia. Mwenye kutubu, mnyonge, Sadiki, amini; Kamwe, kamwe asitengwe Akaaye ndani. Mpya, mwema na mawazo Mwingi wa mapenzi Nawe uwe kielelezo Moyo wa Mwokozi. Ni uule moyo wako; Moyo wa huruma Yesu, natamani kwako Kukujua vyema. Na ya midomo matunda Yako, nipe nami; Amani isiyokoma Iwe yangu mimi. Nitie yako tabia, Inishukie juu; Jina lako nipe pia, Ndilo la upendo. Ni wa baba utukufu; Mwana atukuke; Na roho Mtakatifu U utatu pweke.Ты - песнь моя hyạ nrtl bạlthlyl 主我有一事求你 Sen Tak Mudah Jalanku الله أمين وأب صالح بو دونیَه بَش گونلوک عُمور! Vezi cum zilele se duc şi anii trec Io non ti deluderò ئەي بارچە خەلقلەر
Song not available - connect to internet to try again?