Njoni na furaha, enyi wa imani, Njoni Bethilehemu upesi ! Amezaliwa jumbe wa Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga, Amekuwa radhi kuzaliwa; Mungu wa kweli, wala si kiumbe; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu, Mbingu zote na zijae sifa; Sifuni Mungu aliye Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. Ewe Bwana mwema, twakubarikia, Yesu, utukufu uwe wako; Neno la Baba limekuwa mwili; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.Padre Nuestro Celestial J'ai juste quelques mots Scendi qui Молитва о мире ạ̹tbnạny rḍy by Арслан Przybieżeli do Betlejem سمعت صوت عظيم Rejoice, O Pilgrim Throng ฉันได้รับสายน้ำ I've Got a River
Song not available - connect to internet to try again?