Twendeni askari, watu wa Mungu; Yesu yuko mbele, tumwandame juu. Ametangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini. Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu. Jeshi la Shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia, Kelele za shangwe zivume nchi; Ndugu inueni zenu sauti. Kweli kundi dogo, watu wa Mungu Sisi na mababa tu moja fungu. Hatutengwi nao, moja imani, Tumaini moja, na moja dini. Haya mbele watu nasi njiani, Inueni myoyo, nanyi sifuni; Heshima na sifa ni ya Mfalme, Juu hata chini, sana zivume.Благодарю Тебя Господь из Назарета Таны нэр Беги KA HNGAK THIUTHEO مجد الرب في وسطنا أدخل أمامك Господ ни сравнява с виделина เรานมัสการ We Worship You ạ̉sẖbʿt nfsy̱ За тебе се моля
Song not available - connect to internet to try again?