Yesu aliniita, 'njoo, Raha iko kwangu, Kichwa chako ukilaze Kifuani mwangu.' Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka; Nikapata kwake raha, Na furaha tena. Yesu aliniita, 'njoo, Kwangu kuna maji, Maji ya uzima, bure, Unywe uwe hai, ' Nilikwenda kwake mara Na maji nikanywa: Naishi kwake, na kiu Kamwe sina tena. Yesu aliniita, 'njoo, Dunia ni giza, Ukinitazama nuru Takung'arizia.' Nilikwenda kwake mara Yeye jua langu, Ni kila wakati mwanga Safarini mwangu.Рəбби севəн хилас олаҹаг O serce, wstań i śpiewaj Seninle Babam Göyü yaratmışdır Allahın əli Господь Ты мой свет يسا پاتشا tsbyḥ tsbyḥ tsbyḥ llrb هل كنت تعلمين СУРУДИ ЛАГЕР Здесь, сейчас
Song not available - connect to internet to try again?