Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwangu, Ni mimi kwa kuwa wake, Na yeye kuwa wangu, Ni mimi kuwa wake, Na yeye kuwa wangu Mbingu zinang'ara juu, Na nchi nayo vivyo; Macho ya dunia tu Hayajaona hivyo; Nyuni huimba sana, Maua yana rangi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi, Mambo mengi maovu Nayo yenye kutisha, Sasa hayana nguvu, Si yenye kututisha; Ni mkononi mwake, Nalindwa salamani Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini. Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini. Wake hata milele, Si kutengana tena; Hunipa raha tele Moyoni mwangu, Bwana; Hiyo nchi na Mbingu Zitatoweka zile, Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele. Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele.yạ sẖms dwmy في نهاية الحكاية Ты над всей землёй царствуешь вовек Дързост, братя Oslavuj, Pána oslavuj Бак бу дюня, не дюня Взглянь страдалец на Христа mjdk yʿlạ من يصعد إلى جبل الرب Jeshua
Song not available - connect to internet to try again?