Mwokozi umeokoa, Nimekuwa wako wewe. Damu imenisafisha. Sifa kwa mwana Kondoo. Utukufu, Aleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu! Nilijitahidi sana Ila sikupata raha; Bali kwa kumtegemea Nilipata Baraka. Daima namwegemea Damu ikifanya kazi, Nikioga kwa chemichemi Itokayo Mwokozi. Sasa nimewekwa wakfu; Nitaishi kwako wewe: Fahari nashuhudia Ya wokovu wa bure. Nasimama kwake Yesu, Ameponya roho yangu; Ameniondoa dhambi, Anifanye mzima. Nilikuwa kifungoni, Niliteswa na dhambi, Nilifungwa minyororo Yesu akanifungua. Sifa, ameninunua! Sifa, nguvu za wokovu! Sifa, Bwana huhifadhi! Sifa zake milele.Ofarin Senga - Hudo lmạdẖạ nḥn fqrạʾ wạ̹lhnạ gẖny Senin İşin Görkemlidir Да славит Тебя fy qryẗ hạdyẗ Склонился день к закату الرب إلهنا فى وسطنا 我们要称谢 Песня Ангела رەببىم ئەيسا مەسىھ بىلەن ماختىنىمەن
Song not available - connect to internet to try again?