Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa, Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa; Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa; Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa. Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe katika damu; Takuwa safi kabisa. Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini, Na maumivu si haba yaliyompata chini. Nataka kijito hicho niende kuoga sasa; Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa. Safi kabisa; safi kabisa! Ndicho kinitakasacho, Nami ni safi kabisa. Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu; Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu? Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa; Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa. Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe kwa damu yako, Nami ni safi kabisa.S Bohom začínam zas deň Un jour dans tes parvis ىيسا ۔ جەڭىش ەەسى، ىيسا ۔ جەڭىش ەەسى حبيبي أمين Світи зірко Віфлеємська Aw Kalvari! Исо Масиҳ Подшоҳимиз Ka Pa In Vangsakna Seluruh Alam Tak Henti Апирин Саңа Рәб Әйса
Song not available - connect to internet to try again?