Ninaye Rafiki naye Alinipenda mbele; Kwa kamba za pendo zake Nimefungwa milele; Aukaza moyo wangu, Uache mageule, Mimi wake, yeye wangu; Ndimi naye milele. Ninaye rafiki ndiye Aliyenifilia; Alimwaga damu yake Kwa watu wote pia; Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele; Pia vyote ni amana Ndimi wake milele. Ninaye rafiki naye Uwezo amepewa; Atanilinda mwenyewe, Juu tachukuliwa; Nikitazama Mbinguni, Hupata nguvu tele; Sasa natumika chini, Kisha juu milele. Ninaye rafiki naye, Anao moyo mwema; Ni mwalimu, kiongozi, Mlinzi wa daima; Ni nani wa kunitenga Na mapenzi ya mbele? Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele.What A Friend - Music lmạ dʿạny rby Сенинле Мутлуйум MY JESUS, I LOVE THEE Иисус моя надежда Io ritornerò İsa, Sen Kurtarıcımsın ạ̉nt ʿạrfny رفعت عيني إلى الجبال Карарлъйъм
Song not available - connect to internet to try again?