Yesu nakupenda, U mali yangu, Anasa na dhambi sitaki kwangu; Na Mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia. Ulipoangikwa Msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. Niwapo hai, niwapo maiti, Kupendana nawe kamwe siachi; Hari za kifo zikinienea, Sasa nakupenda, kuzidi pia. Mawanda mazuri, na masikani Niyatazamapo huko Mbinguni, Tasema na taji nitakayovaa Sasa nakupenda, kuzidi pia.Амьдралын утга учрыг - Зөвхөн Та Мои уста поют хвалу Worthy of my all Vydaj sa úprimne Pánovi Come To Me Шул заман Yükünü Rab'be bırak Вдали от тьмы земных сует Есть Имя у любви Qué hermosos son los pies
Song not available - connect to internet to try again?